Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko Somalia yanaiweka amani ya nchi hiyo njia panda

Machafuko Somalia yanaiweka amani ya nchi hiyo njia panda

Ripoti ya kamati ya baraza la usalama kuhusu Somalia na Eritrea iliyowasilishwa leo inasema shughuli za kuleta amani na usalama nchini Somalia zinakabiliwa na vizingiti vingi ukiwemo ufisadi katika taasisi za serikali.

Mambo mengine ni pamoja na uwezo mdogo wa serikali ya mpito kulipa mishahara maafisa wake na majeshi yamejikita katika ufisadi, na wakati mwingine yanauza silaha hata kwa maadui. Misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula imekuwa ikielekezwa kwa majeshi badala ya raia walengwa.

Na hali hii ni kutokana na watu waliochukua kandarasi ya kuzasambaza chakula hicho ambao wanajinufaisha wenyewe na pia kukiuza kwa makundi ya wanamgambo wenye silaha. Na majirani wote wa Somalia, ikiwemo Djibout, Ethiopia na Kenya wanajihusisha kijeshi kwa njia moja au nyingine kwenye mgogoro wa Somalia na wale ambao bado, basi wana mipango ya kufanya hivyo.