Skip to main content

Mawaziri wa hali ya hewa wa Afrika kukutana kwa mara ya kwanza

Mawaziri wa hali ya hewa wa Afrika kukutana kwa mara ya kwanza

Mawaziri wanaohusika na masuala ya hali ya hewa kutoka barani Afrika watakutana kwa mara ya kwanza katikati ya mwezi Aprili kuanzia tarehe 12 hadi 16 mjini Nairobi Kenya.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa ,mkutano wao utakuwa ni wa kujaribu kuimarisha suala muhimu la utabiri wa hali ya hewa.

Akifafanua umuhimu wa mkutano huo mkuu wa shirika la kimataifa la hali ya hewa Michel Jarraud amesema nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na matatizo ya hali ya hewa.