Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upinzani Sudan walalamika kwa Ban Ki-moon kuhusu uchaguzi

Upinzani Sudan walalamika kwa Ban Ki-moon kuhusu uchaguzi

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Umma Reform and renewal Party (URRP) nchini Sudan Mubarak Al-Fadil amemtumia barua rasmi ya malalamiko katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Malalamiko hayo ni dhidi ya Ray Kenedy ambaye ni mkuu wa masuala ya uchaguzi wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan . Mvutano umezuka juu ya mchakato wa kutoa tenda ya uchapishaji wa karatasi za kupigia kura kwenye uchaguzi unaotarajiwa mwezi Aprili.

Bwana Al-Fadil anasema suala hilo linafungua milango ya kuwepo udanganyifu, kwani awali karatasi hizo zilikuwa zichapishwe nje, na sasa tenda imepewa idara ya uchapishaji ya Sudan inayomilikiwa na chama tawala cha National Congress Party (NCP)