Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia yaanza kupiga hatua kuelekea amani ya kudumu

Somalia yaanza kupiga hatua kuelekea amani ya kudumu

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Ahmedou Ould-Abdallah ameipongeza serikali ya mpito ya Somalia na kundi la Ahlu Sunnah wal Jamaa kwa kutia saini rasmi makubaliano ya amani kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Makubaliano hayo ni nia ya pende zote mbili kuzingatia mkataba wa Djibout wa kushirikiana kikamulifu katika kuleta amani na maridhiano. Amesema anawapongeza pande zote kwa hatua yao ambayo imezingatia maslahi ya Somalia na watu Wasomalia, kwa faiada ya utu wa Somalia.

Na ameongeza kuwa hatua hiyo inaashiria kuwa mabadiliko yanawezekana na mambo yanabadilika nchini Somalia. Makubaliano hayo yamefikiwa kwa kuzingatia mpango wa amani wa Djibout na kufuatia kutia saini mkataba baiana ya serikali na Ahlu Sunnah wal Jamaa tarehe 21 June 2009 mjini Nairobi Kenya mbele ya Umoja wa Mataifa.

Bwana Abdallah amezishukuru pande zote husika na waliofanikisha hatua hiyo, pia amewaalika marafiki wote wa Somalia kusaidia katika ukweli huo wa kuzaliwa upya taifa la Somalia.