Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezindua jopo la kuangalia masuala ya kulinda amani

UM umezindua jopo la kuangalia masuala ya kulinda amani

Umoja wa Mataifa unaimarisha mipango yake ya kulinda amani kwa kuanzisha jopo la ushauri litakalotathmini shughuli za kimataifa za kulinda amani.

Jopo hilo litaongozwa na Jean-Marie Guehenno katibu mkuu wa zamani wa shughuli za kulinda amani.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amechagua wajumbe wa jopo hilo ambao majina yao yametajwa leo, yakijumuisha maafisa kutoka katika vitengo mbalimbali wakiwa na uzoefu wa masuala ya migogoro na uelewa mkubwa wa Umoja wa Mataifa na nchi wanachama wake.

Lengo kubwa la hatua hiyo ni kuimarisha uwezo wa Umoja wa Mataifa wa kuchukua hatua kusaidia baada ya machafuko na ni katika kutekeleza ajenda ya Bwana Ban ya ripoti ya 2009 ya kurejesha upya amani baada ya vita.