Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yanazidi kukatili maisha ya watu Somalia

Mapigano yanazidi kukatili maisha ya watu Somalia

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema watu zaidi ya 70 wameuawa wiki hii kufuatia mapigano makali baiana ya vikosi vya serikali ya mpito ya Somalia na wanamgambo mjini Moghadishu na hasa juzi na jana.

Watu wengine 150 wamejeruhiwa na maelfu kuyakimbia makazi yao. Hali hii imeongeza wasiwasi pia huku kukiwa na taafira kuwa vikosi vya serikali vinapanga mashambulizi makubwa dhidi ya wanamgambo ili kurejesha udhibiti wao kusini mwa Somalia.

Duru kutoka nchini Somalia zinasema raia wengi wanaokimbia wanatoka katika wilaya za Hodan, Howl-Wadaag na Yaaqshiid, na wanakimbilia maeneo yaliyo na usalama kusini mwa nchi hiyo.