Skip to main content

Mafuriko makubwa yamewaacha maelfu bila makazi Kenya: OCHA

Mafuriko makubwa yamewaacha maelfu bila makazi Kenya: OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Kenya zimesababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo na kuwaathiri watu takribani 10,000.

Mafuriko yamearifiwa katika wilaya tisa za maeneo ya kaskazini, kaskazini mashariki na magharibi mwa Kenya. Watu kumi na moja wamearifiwa kufariki dunia hadi sasa, miundombinu imeharibiwa vibaya na mamia ya mifugo na mashamba ya watu yamesombwa na mafuriko.

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya linawasaidia waathirika na vifaa vya malazi.