Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kusaidia kufufua mchakato wa uchaguzi Ivory Coast

UM kusaidia kufufua mchakato wa uchaguzi Ivory Coast

Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast leo amekutana na rais mpya wa tume ya uchaguzi katika nia ya kuupa nguvu mchakato wa uchaguzi, ambao umecheleweshwa zaidi na maandamano na kuvunjwa kwa serikali mwezi uliopita.

Mwakilishi huyo Y.J. Choi amemwambia rais huyo mpya wa tume ya uchaguzi na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Issouf Bakayoko, pamoja na mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI ataisaidia tume hiyo katika maandalizi ya uchaguzi.

Mkutano wao umefanyika siku moja baada ya bwana Choi kusema njia pekee ya kuzuia kudhoofika zaidi kwa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ni kufufua shughuli zake haraka iwezekanavyo.