Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unahitaji dola milioni 59 kuwasaidia wakimbizi wa DR Congo

UM unahitaji dola milioni 59 kuwasaidia wakimbizi wa DR Congo

Umoja wa Mataifa na washirika wake leo umezindua wito wa kuomba dola zipatazo milioni 59 ili kusaidia mahitaji ya haraka ya wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wakimbizi hao wamekimbia vita katika jimbo la Equatorial nchini congo tangu mwezi Oktoba 2009 na wamepata hifadhi ya ukimbizi katika Jamhuri ya Congo.

Fedha hizo ambazo zimeanza kukusanywa tangu Januri na zitaendelea hadi Desemba mwaka huu zitawasaidia wakimbizi elfu 11,  ambao asilimia 80 ni wanawake na watoto, pia wenyeji wa Jamhuri ya Congo katika eneo walipo wakimbizi hao. UNHCR pekee inahitaji dola milioni 20 kati ya fedha hizo.