Mkuu wa Umoja wa Mataifa aruhusiwa kuzuru Gaza

Mkuu wa Umoja wa Mataifa aruhusiwa kuzuru Gaza

Wizara ya mambo ya nje ya Israel jana iliamua kulikubali ombi la katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwakilishi wa sera za nje wa umoja wa Ulaya Catherine Ashton la kuzuru Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo watu hawa wawili wanataka kwenda kutathmini juhudi za misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza. Naibu waziri mkuu wa Israel Silvan Shalom amesema kwamba Israel inataka kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na Wapalestina mara moja.

Bwana Shalom ametoa kauli hiyo kwa waandishi wa habari baada ya kukutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon, kwenye makao makuu ya Umoja huo hapa New York.