Skip to main content

WHO inatoa utaratibu mpya wa kutibu malaria

WHO inatoa utaratibu mpya wa kutibu malaria

Shirika la Afya Duniani WHO linatoa utaratibu mpya wa matibabu ya malaria . Utaratibu huo utakuwa ni wa kwanza ulio salama wa dawa za kuzuia malaria.

Katika miaka ya karibuni tiba mpya ya malaria ijulikanayo kama artemisinin ambayo ni mchanganyoko wa tembe imebadili kabisa matibabu ya malaria, lakini imeelezwa kama hitumiwi ipasavyo dawa hiyo haifanyi kazi.

Utaratibu mpya wa tiba ya malaria wa awamu ya pili ni uthibitisho na mapendekezo ya nchi ambazo zimeathirika na malaria na kupata tiba. Dr Rob Newman mkurugenzi wa program ya kimataifa ya malaria anaeleza tofauti iliyopo baina ya na utaratibu wa awamu ya kwanza uliotolewa 2006 na huu mpya.