Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imelazimika kupunguza nusu ya mgao wa chakula mashuleni nchini Ivory Coast

WFP imelazimika kupunguza nusu ya mgao wa chakula mashuleni nchini Ivory Coast

Mpango wa chakula duniani WFP leo umesema umelazimika kupunguza nusu ya mgao wa chakula mashuleni kwa watoto zaidi ya lakini nne na nusu nchini Ivory Coast kutokana na upungufu wa fedha.

WFP imesema inahitaji haraka dola milioni sita ili kurejesha mgao kamili wa chakula na kuendelea kuwalisha watoto wenye utapia mlo. Mwezi uliopita WFP ilipunguza nusu ya kipimo cha kawaida cha chakula kwa watoto wa shule za msingi.

WFP inasema chakula kitapunguzwa zaidi au hata kuacha kugawiwa kabisa endapo haitopata msaada wowote wa fedha kuanzia mwezi wa April.