Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka marekebisho ya uwiano baina ya wakulima wadogo na wafanya biashara

UM wataka marekebisho ya uwiano baina ya wakulima wadogo na wafanya biashara

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki ya chakula Oliver De Schutter amesema biashara ya kilimo inaweza kuwa kiungo muhimu katika kutambua haki ya chakula.

Amesema mataifa yanatakiwa kuwaunga mkono na kuwasaidia wakulima wadogo wadogo na kushinikiza ushirikiano kubadilisha bei zao na sera . Ameyasema hayo leo katika ripoti yake ya kila mwaka kwenye baraza la umoja wa mataifa la haki za binadamu.

Ripoti hiyo imehitimisha kwamba katika utandawazi huu wa kimataifa ambapo sekta ya chakula inatawaliwa na mashirika makubwa wakulima wadogowadogo wanakuwa na wanunuzi wachache na hawana usawa katika masuala ya upangaji wa bei ya mazao yao jambo ambalo linaleta athari kubwa katika masuala ya haki za chakula.