Skip to main content

Idadi ya waliokufa Haiti haijaongezeka na misaada inaendelea kupelekwa

Idadi ya waliokufa Haiti haijaongezeka na misaada inaendelea kupelekwa

Ofisi ya kuratibu masauala ya kibinadamu OCHA inasema kwamba idadi ya watu waliouawa kwenye tetemeko la ardhi la Januari 12 nchini Haiti haijabadiliaka.

Idadi ya walioathirika ambao kwa sasa wanaishi kwenye makazi ya muda inakadiriwa kuwa milioni 1.3 huku wengine zaidi ya laki sita wamearifiwa kuondoka mjini Port-au-Prince na kuelekea maeneo mengine nchini humo.

Kwa upande wa malazi OCHA inasema lengo ni kuipatia kila familia hema ifikapo tarehe mosi May mwaka huu. Mahema mengine zaidi yanatarajiwa kuwasili Haiti mwishoni mwa mwezi huu.