Skip to main content

Afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda akana mashitaka ya mauaji ya kimbari

Afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda akana mashitaka ya mauaji ya kimbari

Aliyekuwa afisa wa jeshi la Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 leo amekanusha mashitaka ya kuhusika na mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Idelphonse Nizeyimana ambaye alikuwa ni mkuu wa kitengo cha upelelezi na wa pili kutoka ngazi ya juu ya jeshi, katika eneo la Butare leo alipanda kizimbani kwa mara ya pili. Mara ya kwanza alipopanda mahakani mwezi Oktoba mwaka jana Nizeyimana alikanusha makosa yote manne ya mauji ya kimbari, kuchagiza mauaji na uhalifu dhidi ya ubinadamu ikiwemo ubakaji na vitendo vya kikatili.

Mshutumiwa huyo anaedaiwa kutumia mamlaka yake dhidi ya askari na wafanyakzi wengine katika kambi ya Butare, alikuwa ni miongoni mwa wasomi dani ya utawala wa hayati Rais Habyarimana. Anashutumiwa pamoja na mambo mengine kuwatuma askari kwenda kwenye nyumba ya malikia wa zamani wa Rwanda Rosalie Gicanda, ambaye ni ishara muhimu kwa Watutsi wote na kuamuru auawe jambo ambalo lilitekelezwa.

Upande wa mashitaka unadai kwamba Nizeyimana alituma askari kuwashambulia yatima ambao walikuwa wametolewa kutoka kituo cha msalaba mwekundu cha Kacyiru.Nizeyimana alikamatwa mjini Kampala Uganda oktoba 5 mwaka 2009 na akahamishiwa kwenye mahakama ya umoja wa mataifa ya ICTR iliyoko Arusha Tanzania.