Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICRC kukabidhi nyaraka za kihistoria za enzi ya ubaguzi Afrika ya Kusini

ICRC kukabidhi nyaraka za kihistoria za enzi ya ubaguzi Afrika ya Kusini

Kamati ya Kimataifa ya chama cha Msalaba Mwekundu (ICRC) itaikabidhi nyaraka za kihsitoria kuhusu ziara yake ya jela wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, kwa jumba la makumbusho la Roben Island mjini Cape Town hapo kesho.

Nyaraka hizo ni za kati ya mwaka wa 1963 hadi mwaka wa 1964, lakini baadhi ya nyaraka zingine haziruhusiwi kounyeshwa kwa umma.

Mkuu wa wajumbe wa ICRC walioko Pretoria Bi Catherine Gendre, amesema tunatumai nyaraka hizi mbali na kuwa na manufaa kwa jumba hili la makumbusho, zitawezesha kusaidia katika utafiti wa kihistoria.