Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yanawazuia raia kupata msaada Darfur

Machafuko yanawazuia raia kupata msaada Darfur

Shirika linaloratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema machafuko yanayoendelea Darfur yanasababisha maelfu ya raia kushindwa kupata msaada wanaouhitaji.

Shirika hilo linasema kuweza kupata fursa ya kuwafikia raia walioathirika na mapigano ndio lengo lao kubwa kwa sasa pamoja na mashirika mengine ya misaada. Wakati msaada umeshawafikia maelfu ya watu katika maeneo mengine ya Sudan , bado watu wengi hawajafikiwa wala kupata msaada katika maeneo ambayo vita vinaendelea Darfur.

Kwa mujibu wa msemaji wa OCHA vita hivyo vilianza tangu mwezi wa Januari mwaka huu na makombora yamekuwa yakivurumishwa katika maeneo matatu ya jimbo la Darfur.