Vyama vya ushirika kuwasaidia wanawake wenye HIV kujikimu Cameroon

25 Februari 2010

Idadi kubwa ya wanawake waishio na virusi vya HIV kaskazini magharibi mwa Cameroon hivi sasa wanashiriki katika miradi ya kujipatia kipato kupitia vyama vya ushirika kwa msaada wa shirika la kazi duniani ILO.

Msaada huo unafadhiliwa na shirika la kimataifa la maendeleo la Sweeden SIDA. Vyama vya ushirika siku za nyuma vimekuwa msaada mkubwa kwa watu wasiojiweza, lakini watu wenye ukimwi wamekuwa wakiachwa nyuma au kutengwa na wakinyimwa mikopo kwa madai kwamba kuwekeza kwa watu hao ambao ni wagonjwa hakuna faida.

Mradi huu ulioanzishwa mwaka jana una nia ya kubadili mtazao huo. Na ILO inaamini kwamba mradi huo utawafaidi wote, watu wanaoishi na virusi vya HIV na jamii zao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter