Skip to main content

UNAIDS kushirikiana na Swaziland kupambana na ukimwi

UNAIDS kushirikiana na Swaziland kupambana na ukimwi

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya ukimwi UNAIDS Michel Sidibe yuko nchini Swaziland katika hatua ya kwanza ya ziara yake ya siku tantu kusini mwa Afrika .

Ziara hiyo ni ya kuangalia maendeleo na changamoto katika kufikia malengo ya kimataifa ya kuweza kuzuia virusi vya HIV, matibabu, huduma na msaada.

Bwana Sidibe pia atatathmini njia njia ya ushirikiano ili kuimarisha juhudi za kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya HIV.

Nchi hiyo ina asilimia kubwa ya watu walioathirika na ukimwi ikikadiriwa kuwa asilimia 26 ya watu wazima wameambukizwa virusi.