Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makambi mapya ya wakimbizi wa Kisomali yafunguliwa

Makambi mapya ya wakimbizi wa Kisomali yafunguliwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema kuanzia Ijumaa ya wiki iliyopita wakimbizi wa Kisomali wameanza kuhamishwa kutoka kwenye makambi ya muda yaliyoko Dolo Ado Ethiopia kwenye mpaka na Somalia, kwenda kwenye kambi mpya ya Melkadida kilometa 65 kutoka kwenye kambi za awali.

Msafara wa kwanza wa mabasi 11 na malori mawili yaliyokuwa yamemeba pia mizigo yaliwasafirisha wakimbizi 247 ambao walikimbia machafuko katikati na kusini mwa Somalia wiki chache zilizopita.

Wakimbizi hao ni sehemu ya wakimbizi 7000 wa Kisomali ambao wametambuliwa na serikali ya Ethiopia kwa msaada wa wataalamu wa UNHCR. Melkadida ni moja ya makambi tano Kusini mashariki mwa Ethiopia zinazohifadhi wakimbizi wa Kisomali.