Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yafuatilia kwa makini maafikiano ya kusitisha vita Yemen

UNHCR yafuatilia kwa makini maafikiano ya kusitisha vita Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema limetiwa moyo hadi sasa na maafikiano ya kusitisha mapigano ambayo yamedumu kwa muda baiana ya vikosi vya serikali na vuguvugu la Al Houti kaskazini mwa Yemen tangu kutiwa saini mwezi August mwaka jana.

Machafuko hayo yalianza miaka sita iliyopita. Mkataba huo wa kusitisha vita umeanza kutekelezwa Alhamisi iliyopita na awamu ya kwanza imeshaanza kufanyiwa kazi.

Jitihada kama hizo za awali zote zilishindwa kuzaa matunda na mkataba kuvunjika. Mapigano makali ya zaidi ya miezi saba kwenye jimbo la Saada yameongeza mara mbili idadi ya wakimbizi wa ndani nchini humo na kufikia 250,000.