Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka kuwepo utulivu Darfur baada ya machafuko

UM wataka kuwepo utulivu Darfur baada ya machafuko

Mkuu wa vikosi vya pamoja vya kulinda amani vya Umoja wa afrika na Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur Sudan leo ametoa wito wa kuwepo na utulivu kutoka kwa pande zote ,baada ya kuzuka kwa machafuko yaliyosababisha mauji na maelfu ya watu kuachwa bila makazi katika siku za karibuni.

Mapigano ya aina hiyo ambayo yametokea kwenye eneo la Jebel Merra kusini mwa Sudan na Jebel Moon magharibi mwa Darfur amesema mkuu huyo wa UNAMID bwana Ibrahim Gambari, yanaweza kuathiri saana mchakato wa amani unaoendelea ambao kwa kiasi umepiga hatua ya kuelekea kuleta utulivu katika jimbo hilo.

UNAMID kwa sasa inashirikiana kwa karibu na mashirika mengine ya misaada ili kuwasaidia maelfu ya watu waliokimbia nyumba zao.