Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa dharura wa kuwalisha watoto umeanza Haiti

Mpango wa dharura wa kuwalisha watoto umeanza Haiti

Shirika la Afya Duniani WHO linasema mpango wa dharura wa kuwalisha watoto wa chini ya umri wa miaka miatno , wanawake wajawazito na kina mama wanaonyonyesha umeaanza nchini Haiti.

Mpango huo utatoa chakula chenye virutubisho vya hali ya juu kwa makundi hayo ya watu ili kuzuia matatizo ya utapia mlo. Mpango huo unalengo la kuwafikia wanawake elfu 16 na watoto elfu 53.

WHO inasema hakuna ongezeko la maradhi ya kuambukiza ingawa kulikuwa na visa vichache vya homa ya matumbo. Paul Garwood wa WHO anafafanua kuhusu mpango huo wa lishe.