UM waelezea wasiwasi wake kuhusu vifo zaidi vya raia Somalia
Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa makazi na masuala ya kibinadamu nchini Somalia Mark Bowden leo amelelezea hofu yake kufuatia idadi kubwa ya mauaji ya raia na wengine kwa maelfu kukimbia nyumba zao kutokana na mapigano ya hivi karibuni mjini Moghadishu.

Kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita pekee raia zaidi ya 80 wameuawa na wengine zaidi ya elfu nane wamekimbia nyumba zao.Mapigano ya hivi karibuni yametokea kaskazini mwa mji wa Moghadishu hususani wilaya za Heliwa, Yaaqshiid na Wardhiigleey, na huko ndio maeneo ambayo watu wengi wamekimbilia.