Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitendo vya kuwashirikisha watoto vitani vinaendelea DRC

Vitendo vya kuwashirikisha watoto vitani vinaendelea DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema licha ya juhudi zinazofanyika kukomesha ushiriki wa watoto vitani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, bado watoto wanaendelea kupatiwa mafunzo ya kushiri vita katika pande zote, jeshi la serikali na makundi ya waasi.

Shirika hilo linasema wasichana ndio walio katika hatari zaidi ya kuwa watumwa wa ngono na sio rahisi kuachiliwa kama ilivyo kwa wavulana. Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Goma mashariki mwa Congo ,UNICEF imesema watoto wanatumika kama wanajeshi, wafanyakazi na watumwa wa ngono. Taarifa hii imetolewa mwishoni mwa wiki katika kuazimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto jeshini.