Ban Ki-moon apongeza kuachiliwa kwa kiongozi wa upinzani Myanmar

Ban Ki-moon apongeza kuachiliwa kwa kiongozi wa upinzani Myanmar

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza kuachaliwa kwa mmoja wa viongozi muhimu wa upinzani nchini Myanmar baada ya kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani kwa miaka sita, na kusema anatumaini hatua hiyo itasaidia kuwa na mchakato mzuri wa kisisa nchini humo.

U Tin Oo ambaye ni makamu wa Rais wa chama cha Nationa League for Democracy (NLD) aliachuliwa mwishini mwa wiki mjini Yangon baada ya muda wa kifungo chake cha nyumbani kukamilika. Kuachiliwa kwake kumefanyika siku mbili tuu kabla ya leo kuwasili ,nchini humo muwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu Tomas Ojea Quintana.

Bwana Ban anatumai hatua hii itachangia kuwepo kwa mazungumzo baina ya chama cha NLD na serikali ya Myanmar kama moja ya hatua muhimu yakuwepo na siasa za kujumisha pande zote nchini humo.