Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO imeanzisha nyenzo kusaidia masuala ya chakula Haiti

FAO imeanzisha nyenzo kusaidia masuala ya chakula Haiti

Kufuatia kupanda kwa bei ya chakula na upungufu mkubwa wa chakula nchini Haiti kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba nchini hiyo tarehe 12 mwezi uliopita, shirika la chakula na kilimo duniani FAO limeanzisha nyenzo maalumu itakayoyaongoza mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali yaani NGO\'S ambayo yanajihusisha na masuala ya chakula nchini humo.

Nyenzo hiyo itakusanya takwimu kutoka vyanzo mbalimbali na kuwasilisha taarifa hizo katika mfumo wa mawasiliano wa kuchangia na kubadilishasna taarifa. Masuala yatakayogusiwa ni pamoja na barabara zitakazotumika, msimu wa mazao, matumizi ya ardhi, maeneo ya kuishi na taarifa potofu.