Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa kimataifa wa maendeleo wathirika kiuchumi

Mfumo wa kimataifa wa maendeleo wathirika kiuchumi

Mfumo wa kimataifa wa kuchagiza uchumi ulio chini ya mkataba wa ushirikiano (PCT) umeporomoka kwa aslimia 4.5 mwaka jana 2009, ikiwa ni kasi kubwa kuliko ilivyokuwa kwa baadhi ya nchi zilizoendelea na pia tofauti na kukua kwa uchumi kwa baadhi ya nchi za Asia Mashariki.

Takwimu za awali zinaonyesha kuwa maombi ya kimataifa 155,900 yaliwasilishwa mwaka jana , ikilinganishwa na karibu maombi 164,000 yaliyowakilishwa mwaka 2008. Hata hivyo kupungua huko kwa maombi ya PCT sio kubaya saana kama ilivyodhaniwa awali. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa WIPO Francis Gurry hali hii inamaanisha kwamba PCT inafanya biashara nzuri licha ya matatizo ya kiuchumi na kuendelea kulinda maslahi ya kimataifa.