Skip to main content

FAO yawataka wahisani wa kimataifa kuisaidia uwekezaji Haiti wa dola milioni 700:

FAO yawataka wahisani wa kimataifa kuisaidia uwekezaji Haiti wa dola milioni 700:

Shirika la chakula duniani FAO limewatolea wito wahisani wa kimataifa kuunga mkono mpango wa uwekezaji wa dola milioni 700 katika sekta ya kilimo ya Haiti.

 Mpango huo umependekezwa na serikali ya Haiti ili kukabiliana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi, hasa katika miundombinu, pia kuinua uzalishaji wa chakula kitaifa na kutoa ajira kwa watu waliokimbia Port-au-Prince.

Nchini Haiti kilimo kinaweza kuwa chanzo cha ajira ya maelfu ya watu, kuwapatia kipato na pia matumaini. Kama anavyosema Bi Cristina Amaral mkuu wa huduma za dharura kisiwani humo.