Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanaokabiliwa na njaa Sudan Kusini yaongezeka mara dufu

Idadi ya wanaokabiliwa na njaa Sudan Kusini yaongezeka mara dufu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekuwa likitoa msaada wa dharura wa chakula kwa watu takribani lakini tatu katika maeneo mbalimbali ya Sudan Kusini.

Lakini hali halisi inaonyesha kwamba takribani watu milioni 4.3 katika eneo hilo watahitaji msaada wa kabla ya kuanza masika, katika miezi michache ijayo. WFP inasema mazao na mavuno katika eneo la Sudan Kusini hayajapatikana kama ilivyotarajiwa.

WFP ina mpango wa kuwasaidia kwa chakula watu wa Sudan Kusini kwa kipindi cha miezi miwili hadi minane kwa mwaka huu ,ikitegemea mvua zitakuwa kubwa akiasi gain na pia bei cha chakula katika masoko nchini humo. Emilia Casella ni msemaji wa WFP:

(AUDIO) Mara nne zaidi , watu wa Sudan Kusini watahitaji aina fulani ya msaada wa chakula kwa mwaka ujao tofauti na mwaka jana. Kwa ujumla tunatarajia watu million 4.3 wa Sudan Kusini watahitaji msaada wa chakula, idadi ambayo imeongezeka kwa milioni moja ikilinganishwa na mwaka jana. Kama ilivyo katika eneo lingine la pembe ya Afrika kumekuwa na ukame na mazao hafifu.