Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inawasaidia wakimbizi wanaorudi Angola

IOM inawasaidia wakimbizi wanaorudi Angola

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM, huko Angola litatoa msaada wa dharura kuimarisha usalama wa chakula na viwango vya lishe kwa jamii ambazo zinakabiliwa na hatari kutokana na idadi kubwa ya watu wanaorudi nyumbani na maafa ya kimaumbile.

Mradi utatoa msaada kwa karibu familia elfu moja 15 wanaokabiliwa na upungufu wa chakula katika vijiji huko jimbo la Huambo, kwa kuwapatia vifaa vya kuwawezesha kufanya biashara zao binafsi na kilimo. Mradi huo unafanyika kutokana na msaada wa euro laki tisa kutoka kwa idara ya ushirikiano wa kimataifa ya Hispania.