Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongaano la Umoja wa Mataifa lanuia kwarejesha pamoja raia wa Chad

Kongaano la Umoja wa Mataifa lanuia kwarejesha pamoja raia wa Chad

Leo Januari sita Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP), kwa mara ya kwanza limewakutanisha pamoja jamii, viongozi wa dini, na viongozi wa kijeshi ili kubaini ni kwa njia gani jamii zilizosalia na makovu ya vita zinaweza kuishi pamoja kwa amani mashariki mwa Chad.