Skip to main content

Hali ya wasiwasi katika Equateur (JKK) imefumsha mapigano ya kikabila: OCHA

Hali ya wasiwasi katika Equateur (JKK) imefumsha mapigano ya kikabila: OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kuzuka kwa hali ya wasiwasi hivi karibuni, kwenye Jimbo la Kaskazini la Equateur, katika JKK, baina ya jamii za makabila ya Boba na Lobala. Hali hii inaripotiwa iliripusha mapigano makali ya kikabila mnamo tarehe 04 Novemba (2009) ambapo watu 37 walisemekana waliuawa, jumla ambayo UM inaamini ilikaribia watu 100 waliouliwa kwa sababu ya uhasama.