Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia wakutana Roma kuzingatia mradi wa kupiga vita njaa

Viongozi wa dunia wakutana Roma kuzingatia mradi wa kupiga vita njaa

Mkutanao mkuu wa UM, wa siku tatu unaozingataia udhibiti bora wa akiba ya chaklula duniani, umefunguliwa rasmi leo hii kwenye mji wa Roma, Utaliana ambapo KM Ban Ki-moon, kwenye risala yale alionya kwa kukumbusha mnamo siku ya leo pekee watoto 17,000 watafariki duniani kwa sababu ya kusumbuliwa na njaa - ikijumlisha kifo cha mtoto mmoja katika kila nukta tano za dakika - jumla ambayo kwa mwaka inakadiriwa kukiuka vifo milioni 6 vya watoto, licha ya kuwa sayari yetu imebarikiwa chakula cha kuweza kutosheleza mahitaji ya chakula kwa umma wote wa kimataifa, alisisitiza KM.

Alisema watu bilioni moja ziada sasa hivi hukabiliwa na tatizo la njaa sugu, na aliwasihi wajumbe wa kimataifa waliohudhuria mkutano wa Roma kujitahidi kuchukua hatua za haraka, zenye suluhu ya muda mrefu, kukomesha mzozo wa chakula na njaa ulimwenguni. KM kwenye hotuba yake aliwasilisha hatua za jumla angelipendelea kuona zinachukuliwa kimataifa, kupiga vita janga la njaa, tatizo ambalo linahatarishwa zaidi na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na muongezeko wa idadi ya watu, tatizo linalokadiriwa itakapofika 2050 litaulazimisha umma wa kimataifa kulisha watu bilioni mbili ziada wataohitajia chakula. Idadi hii itajumlisha, kwa wakati huo, watu bilioni 9.1 katika dunia. KM alitilia mkazo ya kwamba bayana hii itahitajia kupandisha asilimia 70 ziada ya chakula kuweza kukidhi mahitaji hakika yanayotokana na ongezeko la idadi ya watu duniani. Miongoni mwa mapendekezo aliowasilisha KM kwenye risala yake ni ile rai ya kuzidisha uwekezaji kwenye sekta za kilimo, kwa kuwapatia wakulima, hasa katika mataifa yanayoendelea, mbegu za kuoteshea chakula, maji ya kuhudumia shughuli za kilimo, pamoja na ardhi inayofaa kulima ili kuhakikisha kutazalishwa kima cha juu cha mavuno, na kuwawezesha wakulima husika kufikia masoko ili kuuza bidhaa zao bila ya matatizo, na vile vile kuhakikisha biashara ya bidhaa za kilimo kwenye soko la kimataifa huendeshwa kwa haki, hususan kwa niaba ya wakulima wadogo wadogo wanaojumlisha zaidi wanawake wa nchi maskini.