Skip to main content

KM ahimiza vitendo hakika kukomesha silaha zinazodhuru raia

KM ahimiza vitendo hakika kukomesha silaha zinazodhuru raia

Kwenye ujumbe aliotuma Geneva katika Mkutano wa 2009 wa Mataifa Yalioidhinisha Mkataba wa Udhibiti Silaha Maalumu za Kawaida, KM Ban Ki-moon aliyahimiza Mataifa kuendelea kulenga majadiliano yao kwenye zile juhudi za kuimarisha hifadhi bora ya raia dhidi ya madhara yanayoletwa na matumizi ya silaha hizi katili na zisiobagua,

na alipendekeza pia kwa mataifa, yaongozwe na viwango vilivyojumuishwa kwenye Mkataba juu ya Zana za Vita za Mabomu ya Kutawanywa. KM kwenye risala yake aliyapongeza mataifa 110 yaliokwisha kuridhia Mkataba huo, kwa sasa, na kuzihimiza zile nchi ambazo bado hazijaridhia, kufanya hivyo, hususan Kifungu cha Awali na Itifaki husika.