Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo ya nchi zinazoibuka kutoka mapigano yatafutiwa suluhu ya kudumu na UM

Matatizo ya nchi zinazoibuka kutoka mapigano yatafutiwa suluhu ya kudumu na UM

Warsha Maalumu juu ya Chakula na Mizozo ya Kiuchumi kwenye Mataifa Yaliobuka kutoka Mapigano na Vita ulifanyika asubuhi kwenye Makao Makuu.

KM Ban Ki-moon alisema kwenye risala yake mbele ya warsha, kwamba misaada ya kufufua shughuli za kiuchumi na jamii kwenye mataifa yanayoibuka kutoka mazingira ya uhasama, mara nyingi husitishwa mapema sana na wafadhili wa kimataifa, hasa katika kipindi ambacho nchi husika huwa zinahitajia zaidi misaada hiyo kusawazisha maisha ya jamii zao. Alikumbusha kwamba amani ya kudumu, pia hutegemea misaada maridhawa kwa mataifa yalioshuhudia mikwaruzano, mapigano na vita, hususan zile nchi ambazo tangu hapo zikishuhudia uchumi haba na matatizo ya kifedha za matumizi.