Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majambazi wameshambulia kihorera polisi watatu wa UNAMID katika Darfur Magharibi

Majambazi wameshambulia kihorera polisi watatu wa UNAMID katika Darfur Magharibi

Mnamo Ijumamosi iliopita, kwenye eneo la Zalingei, Darfur Magharibi majambazi wasiotambuliwa waliwapiga risasi na kujeruhi walinzi amani polisi watatu, wanaowakilisha Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID), na imeripotiwa hali ya majeruhi wawili kuwa ni mbaya sana kwa hivi sasa.

Walinzi hawa walikuwa wakiongoza msafara wa malori ya taka. Vile vile majambazi waliripotiwa kuiteka nyara gari ya polisi na kukimbia nayo. Hili ni shambulio la pili kutukia katika wiki moja, na UNAMID imerudia tena mwito wake unaoitaka Serikali ya Khartoum, kuharakisha uchunguzi wao ili kukomesha milele matukio kama haya. UNAMID imeeleza kuwa itaendeleza ukaguzi wake wenyewe juu ya tukio hili. Tangu Januari 2008 zaidi ya darzeni moja ya wanajeshi na polisi wa UNAMID waliuawa kutokana na mashambulio ya uadui dhidi yao.