Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Abu Garda ametuhumiwa makosa ya vita na ICC

Abu Garda ametuhumiwa makosa ya vita na ICC

Vile vile tukizungumzia Sudan, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC), ambayo inakutana leo Ijumatatu mjini Hague, Uholanzi imethibitisha kuwepo mashtaka ya makosa ya vita dhidi ya kiongozi wa waasi wa Darfur, Bahr Idriss Abu Garda ambaye anatuhumiwa kuhusika na mashambulio dhidi ya walinzi amani wa Umoja wa Afrika katika Sudan mnamo tarehe 29 Septemba 2007.

Hii ni mara ya kwanza kwa majaji wa Mahakama ya ICC kutoa wito wa kufika mahakamani kwa mtuhumiwa badala ya kutoa hati ya kumshika mshitakiwa husika. Majaji wanatumai Abu Garda atahudhuria mbele ya mahakama kwa hiyari na hakuna haja ya kumshika, kwa sababu anaaminika na mahakama, hasa baada ya yeye kuonekana kuhudhuria kikao cha kuthibitisha mashtaka dhidi yake.