Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu laanzisha tena majadiliano ya jumla ya mataifa wanachama

Baraza Kuu laanzisha tena majadiliano ya jumla ya mataifa wanachama

Majadiliano ya jumla kwenye kikao cha mwaka cha wawakilishi wote, yameanza tena rasmi leo asubuhi hapa kwenye Makao Makuu, kufuatia kikao cha siku nzima cha Baraza Kuu kilichokusanyika Ijumamosi, ambapo wazungumzaji waliowakilisha mataifa 30 waliwakilisha hoja kadha wa kadha kuhusu taratibu wa kusuluhisha masuala yenye kusumbua umma wa kimataifa.

Asilimia kubwa ya wawakilishi wa kimataifa waliohutubia siku hiyo, walitahadharisha juu ya uharibifu unaochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa, uliojiri kwenye maeneo yao, ambao hudhuru zaidi viumbe na mazingira, na kuathiri mfumo dhaifu wa ikolojia. Vile vile wajumbe wa kimataifa walisailia mgogoro wa uchumi ulioshtadi kwa sasa, kwa makali yasiowahi kushuhudia kwa muda mrefu, kwenye soko la kimataifa, na pia kuzingatia masuala mengineyo yanayosumbua kanda mbalimbali za kimataifa.