Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ameridhika na mahojiano ya awali kwenye kikao cha mwaka cha BK

KM ameridhika na mahojiano ya awali kwenye kikao cha mwaka cha BK

KM Ban Ki-moon alifanya mahojianio na waandishi habari kwenye Makao Makuu ya UM, leo asubuhi, na aliwaambia wanahabari kwamba maendeleo makubwa yalipatikana tangu kikao cha 64 cha Baraza Kuu (BK) kuanza rasmi wiki iliopita, ambapo viongozi wa dunia walifikia maafikiano kadha kwenye juhudi zao za kutafuta suluhu ya kuridhisha ya masuala makuu yanayotatanisha ulimwengu wetu, ikijumlisha udhibiti wa madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, ukomeshaji wa silaha za maangamizi za kinyuklia na kwenye mizozo ya kifedha katika soko la kimataifa.

Alisema aliingiwa moyo kuona fungu kubwa la wawakilishi wa kimataifa, walibainisha kwenye hotuba zao imani iliotambua umuhimu wa UM kuwa ndio chombo pekee kinachojumuisha mataifa yote ya ulimwengu, na chenye uwezo wa kukabiliana, kwa mafanikio, mizozo inayotatanisha dunia yetu kwa sasa hivi.