Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watuma misaada ya dharura kwa waathirika wa mafuriko Afrika Magharibi

UM watuma misaada ya dharura kwa waathirika wa mafuriko Afrika Magharibi

Mashirika ya UM yamelazimika kuongeza misaada ya dharura ya kunusuru maisha, kwa watu 600,000 walioathirika na mafuriko yalioenea katika siku za karibuni Afrika Magharibi, ambapo miundombinu iliharibiwa na kuangamizwa na mafuriko ambayo pia yaliharibu maskuli, hospitali na vile vile kugharikisha mashamba na kuangamiza mazao.