Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ayasihi Mataifa Wanachama kuharakisha mapatano ya kukomesha uchafuzi wa hali ya hewa

KM ayasihi Mataifa Wanachama kuharakisha mapatano ya kukomesha uchafuzi wa hali ya hewa

Wiki iliopita KM Ban Ki-moon, alizuru ukingo wa ncha ya Kaskazini ya dunia, kwenye eneo la Akitiki, ambapo alishuhudia mwenyewe athari kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa na kujionea, binafsi, namna miamba ya barafu na michirizi ya barafu inavyoyayuka kwa kasi kabisa kwenye eneo hilo, hali ambayo inachochea kina cha bahari kunyanyuka katika sehemu kadha za dunia, na kuhatarisha baadhi ya mataifa ya visiwa ambavyo huenda vikaangamia ikiwa hali hii haotidhibitiwa mapema.

Kwa mujibu wa taarifa za wataalamu, mabadiliko alioyashuhudia KM katika Akitiki ndio yenye kuharakisha mageuzi haribifu ya hali ya hewa, takriban katika ulimwengu mzima. Katika miaka ya karibuni, eneo la Akitiki, Kaskazini ya dunia limeonekana likinyonya joto na kuyayesha michirizi ya barafu ya baharini badala ya kuakisi joto, hali ambayo inapalilia muongezeko wa halijoto duniani. Utaratibu huu, wataalamu wanasema, husababisha gesi ya mitheni, ilionaswa kwenye uketo wa bahari, kuvuja na kuchafua anga. Gesi hii, wataalamau wanasema, inatoa sumu haribifu ambayo nguvu zake huzidi mara 20 ile gesi ya asidi kaboniki inayochafua anga hivi sasa.

KM baada ya kumaliza ziara ya Akitiki, alihudhuria Mkutano Mkuu wa Tatu juu ya Hali ya Hewa (WCC3) uliofanyika mjini Geneva, Uswiss. Alipohutubia Mkutano aliwasihi wajumbe wa kimataifa kuharakisha mapatano yao ya kuanzisha mkataba mpya utakaosaidia kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, kidharura, au si hivyo, alitahadharisha, kuna hatari ya kuzuka majanga makubwa ya kiuchumi na jamii yatakayozagaa na kuathiri ulimwengu mzima.

KM alionya kwenye hotuba yake kwamba bila ya mataifa kuchukua hatua za pamoja kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa yanayoashiriwa kuzuka katika siku zijazo, kwa kufikia makubaliano ya kuridhisha, kuna hatari ya vizazi vijavyo kukabiliwa na mizozo ya maisha magumu, isio kifani. KM alibashiria ni matokeo ya aina gani yatazuka pindi mataifa yatapwelewa kuchukua hatua za mapema za kudhibiti taathira za mabadiliko ya hali ya hewa, kama ifuatavyo:

CUT: IN: "By the end of this century, sea levels may rise betwn ...

SG/BK OUT: .. when the rains fail or floods wash away the crops?"

WCC3 "Mwisho wa karne hii, kina cha bahari kinatarajiwa

Geneva kunyanyuka baina ya nusu mita mpaka mita mbili .. na

03/09/2009 tusisahau watu milioni 60 hivi sasa tayari wanaishi katika maeneo ya usawa wa mita moja na bahari .. idadi ambayo mnamo mwisho wa karne ya 21 inatazamiwa kuongezeka na kuzidi milioni 130 ya watu watakaokuwa wanaishi kando ya bahari. Umma huu, kwa sasa, hukutikana zaidi kwenye madelta ya mito mikuu katika Afrika na Asia .. na kwenye visiwa vya nyanda za chini. Tujiulize raia wanaoishi kwenye miji ya mwambao watafanya nini dhoruba kuu zikianza kuzisukuma bahari ndani zaidi kwenye nchi? Wapi umma huu utakimbilia? Umma wa Kusini na Kusini-mashariki ya Asia na Uchina watafanya nini pale akiba yao ya maji yanayotoka kwenye Milima ya Himalaya itakapokauka, maeneo ambayo, tusisahau, ndipo wanamoishi karibu nusu ya jumla yote ya watu wa dunia!? Vile vile tusisahau wakulima wa Afrika, tuzingatie pindi mvua zitashindwa kunyesha au mafuriko yatakapogharikisha na kuangamiza mazao yao, tunatarajia umma huu ufanye nini kuepukana na janga hilo? Jawabu ya masuala yote haya imo kwenye ‘ukuzaji wa mazingira ya kijani', ukuzaji unaosarifika, na wenye ustawi utakaonufaisha umma wote wa kimataifa na kuhakikisha walimwengu watakuwa na mkataba mpya utakaotumiwa kudhibiti bora taathira za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni."

Kwa hivyo KM aliwasihi wajumbe wa Mataifa Wanachama kuharakisha maafikiano yao juu ya waraka wa mkataba mpya wa kuzingatiwa kwenye Mkutano wa Copenhagen utakaofanyika mwezi Disemba, maafikiano ambayo yakitekelezwa KM aliamini yatasaidia kuuvua umma na maafa ya kiuchumi na jamii kwa siku zijazo.