Maharamia wa uvuvi watanyimwa makimbilio salama baada ya kufikiwa maafikiano mapya ya kimataifa

Maharamia wa uvuvi watanyimwa makimbilio salama baada ya kufikiwa maafikiano mapya ya kimataifa

Mataifa Wanachama 91 wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) yameafikiana kuukubali waraka wa mwisho wa mkataba wa kimataifa uliokusudiwa kupiga vita uvuvi haramu kwenye maeneo yao.

Lengo hasa la maafikiano haya ni kuhakikisha vyombo vilivyoshiriki kwenye uvuvi ulio haramu, usioripotiwa na usiofuata kanuni (IUU) havitoruhusiwa kuegesha kwenye bandari za mataifa wanachama wa FAO. Maafikiano haya yalisimamiwa na FAO na yatajulikana kama "Mapatano ya Kanuni za Bandari za Mataifa Kuzuia, Kukataza na Kukomesha Uvuvi Haramu, Usioripotiwa na Usiofuata Sheria", na maafikiano haya yatakuwa mkataba wa awali wa dunia utakaoangaza kwenye matatizo ya uvuvi haramu. FAO inatumai maafikiano haya yatasaidia kuzuia samaki waliovuliwa kinyume na sheria kuuzwa kwenye soko la kimataifa na, hatimaye, kuondosha vichocheo vinavyowapatia fursa baadhi ya wavuvi kushiriki kwenye vitendo haramu.