Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtetezi wa Haki za Binadamu aisihi Zambia kwamba "ufukara hauondoshwi na ufasaha wa lugha bali vitendo"

Mtetezi wa Haki za Binadamu aisihi Zambia kwamba "ufukara hauondoshwi na ufasaha wa lugha bali vitendo"

Baada ya kukamilisha ziara yake katika Zambia, Mtaalamu Huru wa UM anayetetea haki za binadamu na umaskini uliovuka mipaka, Magdalena Sepúlveda, kwenye mahojiano na waandishi habari mjini Lusaka alionya kwamba "ufukara mkubwa uliopamba nchini Zambia haotofanikiwa kukomeshwa kwa ufasaha wa usemaji bali kwa vitendo halisi."

Ziara ya Sepúlveda katika Zambia ni ya awali kufanyika na mtetezi wa haki za binadamu wa kutoka UM. Kwenye risala yake Sepúlveda alisema "Zambia ni taifa lenye utajiri wa mali ya asili kadha, taifa ambalo katika miaka 8 iliopita limeshuhudia ukuaji mkubwa wa uchumi." Lakini alisema licha ya maendeleo hayo, ilishtusha kuona umaskini uliovuka mipaka bado umeselelea kwenye majimbo mbalimbali ya nchi. Bayana hii ni ripoti ya awali kuhusu ziara ya Sepúlveda, katika Zambia. Alisisitiza pia kwamba Serikali ya Zambia ilishatoa ahadi ya dhahiri na kuelezea juu ya miradi kadha muhimu ya kurekibisha hali ya ufukara nchini humo. Alitilia mkazo kwamba ahadi za kauli za ufasaha ni lazima zifuatiliwe na vitendo ili kukomesha ufukara uliohanikiza katika taifa.