Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya hali ya hewa yabatilisha historia kuwa ni kiashirio kwa wakulima, anasema Mkuu wa WMO

Mabadiliko ya hali ya hewa yabatilisha historia kuwa ni kiashirio kwa wakulima, anasema Mkuu wa WMO

Michel Jarraud, Mkuu wa Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) amenakiliwa akisema mabadiliko ya hali ya hewa yameifanya tarikh/historia kuwa ni chombo kisio sahihi tena katika kuongoza shughuli za wakulima, pamoja na wale wawekezaji wa kwenye nishati.

Jarraud alisema maji na utabiri wa halijoto unathaminiwa zaidi kwa sasa, kuliko takwimu za kihistoria juu ya hali ya hewa. Alisisitiza kwamba taarifa zilizokusanywa kutoka majira yaliopita haziwezi tena kutumiwa na wataalamu kubashiria siku za baadaye. Alisema kwamba watu wanaoazimia kujenga miundombinu ya nishati kwa sasa huwa wanahitajia wapatiwe taarifa hakika juu ya namna hali ya mazingira itaathiri faida ya muda mrefu ya miradi yao. Wiki ijayo wajumbe zaidi ya 1,000 wanaojumlisha wabunisera, wataalamu watafiti pamoja na viongozi wa mashirika makuu ya kibiashara watakutana mjini Geneva kusailia namna ya kufanya bora ukusanyaji wa taarifa zinazohusu mabadiliko ya hali ya hewa na kugawana matokeo hayo kimataifa.