Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya Afrika Kusini na Misiri vyawasili Darfur kuisaidia UNAMID

Vikosi vya Afrika Kusini na Misiri vyawasili Darfur kuisaidia UNAMID

Mnamo mwisho wa wiki iliopita wanajeshi 95 kutoka Misri pamoja na maofisa wa polisi 79 wa Afrika Kusini waliwasili Darfur kujiunga na Shirika la Ulinzi Amani la UM-UA kwa Darfur (UNAMID).

 Vikosi vya polisi vya Afrika Kusini, vitajumlisha asilimia 70 ya askari wanaohitajika kuendeleza shughuli za polisi katika Darfur. UNAMID liliripoti pia kwamba inatarajia wanajeshi ziada kutoka Misri kuwasili karibuni Darfur, ambao watajiunga na askari wazalendo wenziwao 2200, wanaojihusisha na operesheni kadha za kuimarisha amani katika Darfur