Skip to main content

Watoto wadogo milioni 6 kupatiwa chanjo kinga ya polio katika Cote d'Ivoire

Watoto wadogo milioni 6 kupatiwa chanjo kinga ya polio katika Cote d'Ivoire

Serikali ya Cote d\'Ivoire leo inakamilisha kampeni ya siku nne iliokusudiwa kuchanja watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano, dhidi ya maradhi hatari ya kupooza au polio, shughuli ambazo zilianzishwa rasmi tarehe 14 Agosti.

Shirika la UM Kulinda Amani katika Cote d'Ivoire (UNOCI) lilisaidia kusafirisha timu za wafanyakazi wa afya na vifaa vyao katika maeneo 41 kwenye wilaya za Odienné na Daloa. Watoto milioni 6 walitarajiwa kupatiwa dawa ya chanjo kinga dhidi ya polio. UNOCI itaendelea kuisaidia Serikali ya Cote d'Ivoire katika siku chache zijazo kutathminia juhudi za kuchanja watoto wachanga, juhudi zilizosaidiwa kuhudiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF). Maradhi hatari ya kuambukiza ya polio humpata mtu kwa sababu ya chakula kichafu, maji machafu na vinyesi, maradhi ambayo yalidhaniwa yameshakomeshwa milele nchini Cote d'Ivoire katika miaka ya karibuni. Lakini mwezi Disemba 2008, katika mji wa Adiaké, Cote d'Ivoire ya mashariki, kuligunduliwa kufufuka tena kwa maambukizi ya polio yaliodhuru raia mmoja.