Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo machache yalipatikana kwenye kikao cha Bonn, asema Mkuu wa UNFCCC

Maendeleo machache yalipatikana kwenye kikao cha Bonn, asema Mkuu wa UNFCCC

Mkutano wa wiki moja kuzingatia vifungu vya waraka wa kujadiliwa kwenye Mkutano wa Copenhagen kuhusu udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa, utakaofanyika mwezi Disemba, Ijumaa ya leo, umekamilisha mashauriano yake mjini Bonn, Ujerumani. Wajumbe wa kimataifa 2400 walihudhuria kikao hicho cha Bonn.

Yvo de Boer, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya UM kuhusu Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) alisema "maendeleo machache" yalipatikana mkutanoni licha ya kuwa serikali zilifanikiwa kukubaliana juu ya vifungu vyenye uwezo wa kutekelezwa kimataifa hususan katika marekibisho ya matumizi ya teknolojia itakayodhibiti bora uchafuzi wa hali ya hewa. Kadhalika nchi zenye maendeleo ya viwandani zilitakiwa kuharakisha ile miradi ya kupunguza umwagaji wa hewa chafu kwenye anga.