Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu anaamini makosa ya vita yamefanyika Usomali

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu anaamini makosa ya vita yamefanyika Usomali

Kamishan Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, ameripoti Ijumaa kwamba ana ushahidi thabiti wenye kuonyesha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ulifanyika katika mapigano ya karibuni kwenye mji wa Mogadishu, ambapo pia sheria ya kiutu ya kimataifa iliharamishwa kutokana na vitendo ambavyo anavitafsiri kisheria kuwa ni "makosa ya jinai ya vita".

 Pillay alisema ,miongoni mwa mambo karaha yalioshuhudiwa kupamba kwenye mzozo wa Usomali wa karibuni, ambao umeselelea nchini tangu 1991, ni ile tabia ya kushambulia kihorera raia wasio na makosa. UM umeripoti kwamba wachunguzi wake walipokea ushahidi kutoka raia, waliarifiwa na na madi ya kuwa makundi ya vijana wa Al Shabaab yanayopigana na vikosi vya Serikali ya Mpito, yaliendeleza mauaji ya watu nje ya sheria, na vile vile wametega mabomu kwenye maeneo wanamoishi raia, na hata kudai kwamba waliwatumia raia kama ni ngao ya kiutu kujikinga na mashambulio ya vikosi vya Serikali.