Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inajumuika na mashirika ya kiraia kuhudumia waathirika wa mapigano ya Mogadishu

UNICEF inajumuika na mashirika ya kiraia kuhudumia waathirika wa mapigano ya Mogadishu

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza kujumuika na shirika la Denmark, lenye kuhudumia wahamiaji (DRC) na pia shirika la kizalendo linalohusika na huduma za amani Usomali, SYPD, kwenye shughuli za kusaidia kaya 6,000, sawa na watu 47,000 walioangamizwa katika eneo la Mogadishu.

UNICEF imearifu asilimia kubwa ya watu waliong'olewa makazi (IDPs) Mogadishu wamehamia kwenye eneo la ushoroba wa Afgooye, yalipo makazi ya msongomano mkubwa wa wahamiaji wengine muhitaji 400,000 wanaotafuta salama.

Wahamiaji wote hawa wanatazamiwa kufadhiliwa misaada ya kihali na UM na mashirika yasio ya kiserikali, ikijumlisha maturubali ya plasitiki ya kutumiwa kuekezea vijibanda vya muda, na vile vile kupatiwa mablanketi, majerikeni ya maji, sabuni na vyandarua.